Monday, January 6, 2014

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJIL TANZANIA AIBUA MAZITO


wakati tukiwa ndo tunaanza mwaka mpya wa 2014 huku nako mwimbaji wa muziki wa injili hapa nchi anayefahamika kwa jina la Gazuko ambaye anafanya muziki wa injili kwa style ya kurap na sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa chnguza
amefunguka kwa kutoa mambo yaliyokuwa chini ya kapeti wakati akifanya mahojiano maalumu na blog hii akizungumzia muziki wake ila alifunguka zaidi pale alipoulizwa swali kuhusu wadada ambao huwa wanajifanya wanaimba muziki wa injili alafu mwisho wa siku wa siku wanaonekana katika mitandao ya kijamii wakiwa katika pozi za mitego pamoja na kupiga picha za utupu hivi ndivyo alivyofunguka...
"yeah off course ni ishu ambayo ipo na inanikera sana nakumbuka mwaka wa jana mwanzoni dada mmoja anayeitwa Lissa Mlaki ni mchekeshaji kutoka kundi la vituko show alinipigia simu na kuniambia kuwa nataka nimsaidie jinsi ya kutimiza ndoto zake za kumwimbia Mungu hivyo nikamtafutia mwalimu wa kumfundisha kwa maana alikuwa yupo tanga huku mimi nikiwa dar es salam na aliniambia kuwa ameokoka hivyo nikaenda naye sawa lakini mwishon mwaka mwaka wa jana nilipigiwa simu na rafiki yangu akiniambia nitazame blog fulani kwa kwel nilipotazama nilibaki hoi ila ishu ni kwamba hawa dada zetu waache mchezo wa kumtania Mungu" amesema Gazuko.

No comments:

Post a Comment