Thursday, November 28, 2013

GAZUKO KUACHIA CHUNGUZA WEEK IJAYO


kijana anayefanya vizuri katika anga la muziki wa injili kwa style ya hip hop a.k.a kufoka foka
ambaye anafanya vizuri na track ya Yesu ni Bwana pamoja na Naja mbele zako
huyu si mwingine bali ni Gazuko Mzengaeka ila anafahamika kwa jina la Preacher Gazuko,
Gazuko amezungumza na blog hii na kusema kuwa ndani ya wiki ijayo anatarajia kuachia wimbo
wake mpya baada ya kufanya vizuri na hizo kazi mbili zilizopita,
Pia Gazuko ameongeza kwa kusema kuwa ndani ya wimbo huu ameamua kuwa shirikisha
wakali wengine wa gospel hip hop hapa nchini Tanzania ambao ni Bashando na Mwimba huku chorus
ikiwa imetendewa haki na Shaboka ni wimbo wa tofauti ambao ukiusikiliza ni kama worship flani hivi
bt ni hip hop kwa mujibu wa Gazuko amesema kuwa wimbo huo atautoa kwa mfumo wa audio na utapatikana kwa njia ya internet hivyo watu wote wanaweza kudownload kabla ya jumapili ya tarehe 6 ya mwezi wa 12,
Hivyo amewataka wapenzi wote wa hip hop na sio gospel hip hop tu wakae mkao wa kupokea kile kitu
ambacho Gazuko amewaandalia tunapoelekea kumaliza mwaka 2013 tukamalize na ujio mpya wa Gazuko

No comments:

Post a Comment